Jumatatu 29.06.09 : Unguja
Tunakula chakula cha asubuhi juu ya ghorofa ya hoteli na tunaongea kwa kidachi na mbelgiji mmoja na mholanzi mmoja, wema sana.
Mtandao unapatikana ; kisha tunakwenda katika nyumba hii kununua tiketi mbili za ndege kwenda Moshi. |
Mchana na jioni, tunatembea kati ya mji Mkongwe na vichochoro vingi. |
Unguja inajulikana kwa utalii lakini ninasikitika kidogo.
Kuna vichochoro vingi, vichafu mara nyingi, kuna watu wengi wanatukera wakitualika kuingia dukani na kuna maduka mengi.
Tunaona nyumba nzuri sana na milango ya nakshi.
Isitoshe, kuna pikipiki nyingi na inabidi tugeuke daima.
Nilipenda zaidi kisiwa cha Pemba na desturi ya kweli na watalii wachache.
Lucie alituarifu atakaa hoteli jirani ya hoteli yetu ;
tunakutana na tunatembea nae pamoja na rafiki yake masai. |
yaliyomo