en français en français en français en français

tanzania


Nilipokwenda Rwanda na Tanzania mwaka 2007, Africa inanipendeza sana na nimeazimia kurudi pale. Sasa, sisingizii kwenda kufanya kazi wiki tatu lakini nakwenda kwa utalii tu.
Nilitafuta mtu anayekubali kufuatana nami Tanzania, nikapata majibu mazuri lakini tarehe ya safari ilipokaribia, watu wengi walikataa mwaliko wangu.
Hawakuwa na nafasi, inabidi waondoke kwenda likizo na familia zao, ni muda wa mitihani ya watoto, wana mimba, wanaogopa nyoka, walidhani nilisema mzaha, n.k...
Lakini, nilikuwa na uhakika nikimwambia Noemie atakubali ; kwa hiyo, ninasafiri naye.
Inabidi uzoee ... mimi pia !!!

Mwaka 2007, ni ajabu kwamba watu wengi walipenda sana taarifa yangu ya safari.
Kwa hiyo, ninaandika tena mwaka huu.


Ukibofya katika tarehe mojawapo katika orodha ya mwanzo wa ukurasa huu, unaweza kusoma taarifa ya siku hiyo.
Ukitaka kuongeza au kupunguza ramani za mwendo wa siku moja au ramani za yaliyomo, inabidi ubofye katika ramani.
Chini hapa, ni ramani yote ya Tanzania.



Ukibofya hapa, unaweza kuona picha zote za safari yangu.