Jumanne 30.06.09 : Unguja - Kizimkazi - Ungunja


Noemie anavumbua safari ya kutamanisha kwa leo kwani ndege ya kwenda Arusha itaruka kesho tu.
Tutakwenda baharini kuona pomboo na tutaogelea nao.

Tunafika Kizimkazi na waingereza wawili lakini bahari ni chafu sana.
Tunapanda katika mashua na waingereza, wazungu wawili na wakazi wawili.
Bahari inachafuka sana na urefu wa wimbi ni mita mbili na tunarutubishwa mbio.
Tunatafuta pomboo kwa muda mrefu lakini hatuwakuti.
Baada ya saa moja na nusu ya wimbi, tunarejea ufukweni, tunajikausha na tunakula kidogo.


Viongozi wetu wanatushauri tusimame mwituni ; mbega wanaishi pale tu na ni wema sana.
Huyu yuko karibu nami, toa mita moja.
Kuna mbega wengi na inabidi nisisimame chini ya mbega waliopo juu ya mti ; ninadhani unafahamu sababu !

Kisha, tunafuatana na kiongozi anayetuonyesha mikoko na anatueleza hiyo.

Tunarudi Unguja, kutembea, kunywa na kula pahali pa jana, katika mtaa.
Pahali hapa patabaki kumbusho bora la Unguja.
Usiku, hotelini, hakuna umeme tena na tunakaa na mshumaa.


yaliyomo