Jumapili 28.06.09 : Mkoani - Unguja



Tunakwenda mpaka bandarini kununua tiketi kwa kwenda Unguja.
Ninaomba tiketi za daraja la pili lakini inabidi wageni wasafiri daraja la kwanza tu.
Hapa, daladala nyingi zinafika na watu na mizigo.
Wauzaji wa mji wanauza maji, ndizi, machungwa na vyakula mbalimbali kwa kula melini ; ndizi ni ndogo na tamu sana na bei zake ni shilingi 50 (yuro 0.03).
Safari inakusudiwa kuanza saa nne asubuhi.

Tunakaa daraja la kwanza na ni tofauti sana na daraja la kwanza la meli ya kutoka Tanga kwenda Wete ; Inaonekana, walikuta viti vya ndege na waliweka viti kama katika ndege.
Kwenye luninga inatangazwa hotuba inayodumu saa mbili ; baadaye tunaweza kuangalia filamu ndogo.
Wabelgiji wanahisi kwao kwani maarifa yote yanaandikwa kwa kidachi.

Safari inadumu saa sita na nusu ; kuna mawimbi mengi na ninafurahi kwamba nimemeza dawa inanihifadhi katika ugonjwa wa safari.
Watu wanalala kwenye viti au chini na ni vigumu kwenda nje kwani inabidi tuwaruke.
Kuna kuku na jogoo wanaofungwa mguu mmoja ; muda wa kupanda na kuondoka meli, wanyama hawa wanakaa katika kikapu kidogo na vichwa vyao tu nje.

Ni picha ya kuwasili bandari ya Unguja ; watu wote wanasukumana kwa kuondoka kutoka melini.

Mara moja, wavulana wanataka kutupeleka mpaka hotelini lakini tulipiga simu hotelini kwa kunusuru chumba, na hoteli hiyo ni karibu na bandari.

Tunaweka mizigo na tunatembea ufukweni ; watoto wanacheza na mpira na wanaogelea.
Hapa, kuna watu wengi na wazungu wengi pia.
Ni tofauti sana baina ya hapa na Mkoani shwari.

Tunaona mahali pa kula kesho : kuna maduka mengi na watu wanapika nyama, samaki, pweza, ngisi n.k.


Yaliyomo