Jumamosi 27.06.09 : Wete - Mkoani


Tunaamka saa kumi na moja kasorobo alfajiri, tukaoga, tukala kidogo na tukasubiri basi linalochelewa nusu saa ; inaonekana linajaa sana.
Kuna vituo vichache. Hatimaye, mna watu yapata hamsini (wakiwamo watoto kumi na tano) kwa nafasi ishirini na tatu. Safari inadumu saa moja na nusu.
Hakuna mtu anayeteremka Chake-Chake kwani watu wote wanakwenda Mkoani kupanda meli kuelekea Unguja.
Tunaazimia kwenda Unguja kesho ; pale, tutapanda ndege mpaka Moshi na Noemie atasafiri kwenda porini, na mimi nitabaki peke yangu na nitazunguka karibu na Kilimanjaro.

Hoteli iko kilomita moja toka kituo cha basi na tunakwenda kwa miguu.
Tunakaa nje ya hoteli, mtazamo wa mazingira ni mzuri sana.
Kwa usiku wote wa Pemba, hakuna wanunuzi wengine hotelini.

Tunarejea mpaka bandarini na tunatembea sokoni na ufukweni.
Mitumbwi mingi inafika baada ya kuvua.
Watoto wanatuzinga lakini hakuna watoto wengi wanaoomba pesa.
Tunatembea mjini kwa kununua makubazi lakini tunaona jozi moja ya viatu tu ambavyo ni shupavu mno ; ni matumaini yangu tutatafuta makubazi kesho, Unguja

Ni joto sana sana !
Ninadhani maisha yangu yote, sijahisi joto hivyo ; lakini labda mimi ni mzee zaidi.

Wanawake hawa wanatayarisha vyakula vya asubuhi : samaki au pweza.
Ni vizuri sana na tunakula nje ya hoteli kwa mbele jua linazama.


Yaliyomo