Jumatano 24.06.09 : Wete - Ngezi - Wete

Leo Arifu anakuja kutuchukua na anatuendesha kaskazini ya kisiwa.
Barabara ni mbaya sana.

Tunasimama barabarani kumchukua dada ya dereva yetu na mtoto wake wa miezi sita ambaye ana matatizo na mguu wake.
Tunaingia nyumbani kwa mganga wa watoto, mwanamke wa miaka yapata sitini ; anatibu mtoto mchanga na tunahudhuria anapochua mtoto kwa nguvu.

Tunavuka mwitu mzito mzuri ; ndege wengi na tumbili wanaishi hapa lakini hatuwaoni.
Noemie na Lucie wanapenda zaidi kwenda mwambao na mimi ninatamani kushuka na kutembea kwenye mwitu.
Bahati mbaya, hakuna njia na kuna nyoka wengi na ninaazimia kwenda mpaka bahari ya Hindi na marafiki zangu.

Tunakula pikiniki sote pamoja na wanawake wanakwenda kuogelea na, hasa, kuongea sana baharini ; mimi ninaongea pia kwenye kivuli na dereva wetu.
Baada ya saa mbili na nusu, dereva anatupeleka Wete na kituo kimoja kwake kuchukua kitu na kutuonyesha picha nyingi za yeye na baba yake n.k.

Tunakula hotelini (tuna tena) na tunapumzika kwa sababu tumechoka kwa kuwa hali ya barabara za Wete ni mbaya.


yaliyomo