Jumanne 23.06.09 : Tanga - Wete


Kivuko kuelekea kisiwa cha Pemba kinaondoka mapema.
Inabidi tununue tiketi saa kumi na mbili na nusu alfajiri, tukapanda saa moja na meli inaondoka saa mbili.
Hatuombi kila kitu lakini mtu anatuuzia nafasi za daraja la kwanza.
Ingewezekana kuchagua, tungechagua daraja la pili lakini tunaona hawa wazungu wawili wengine wanakaa pia katika daraja la kwanza, hakuna uchaguzi.
Hapa kuna pangaboi na makoti ya kuokoa na tuna ruhusa kwenda pahali pa daraja la pili na daraja la tatu.
Tunakutana na Lucie, msichana mfaransa anasafiri Tanzania peke yake tangu wiki tatu.

Safari inadumu masaa nne na nusu na, bahati, watu wa daraja la kwanza (na la pili) wanaweza kutumia viti vya anasa kwa kupumzika

Baada ya kufika Wete, tunapita ofisini ya uhamiaji ; wavulana wawili wanatupendekezea kwenda hotelini tuliyochagua (sisi na Lucie) na tunafuatana kwa miguu.

Kwanza tunapewa chumba na kisha, mkazi anayeitwa Beka, anatuonyesha vichochoro na tunaona vibanda vichache.
Hapa watu wapendevu wana tubasamu na wanatukaribisha vizuri.

Noemie na Lucie wanakwenda kuogelea baharini na mimi ninatafuta ofisi ya mtandao na Beka ; inaonekana ofisi itafunguliwa kesho.
Halafu Beka ananipeleka katika nyumba ya mama anayetwanga muhogo na bibi wengine wanaangalia luninga.
Nyumba hiyo ni mkahawa pia na tunakunywa kinywaji ; kiongozi yangu ni mwislamu lakini anapenda sana gin !
Kisha tunakwenda kwake na ninaongea kidogo na mama yake na dada yake.

Baada ya kula vyakula vizuri, marafiki wetu wawili (Kassim na Beka) wanatuendesha mpaka mkahawani na tunaongea sana kuhusu safari yetu ya kesho.
Bei ya ziara ya pwani nzuri inapungua daima ; Noemie na Lucie wanaongea sana na bei ya mwisho ni asilimia sitini ya bei ya mwanzo.


yaliyomo