Alhamisi 25.06.09 : Wete - Chake-Chake - Wete

Leo Hussein ni mtu mwema kama Arifu, kiongozi wa jana. Anatuendesha, mimi na Noemie na Lucie, kugundua viungo vya chakula kisiwani.

Tunapofika kijijini, watoto wazuri wanatukaribisha na wakataka tuwapigie picha nyingi.
Tunatembea kwenye msitu na tunaona viungo vyote vya chakula kisiwani : karafuu, mdalasini, hiliki, ukwaju, vanila, mlangilangi, tangawizi, manjano, pilipili manga, n.k.
Inatamanisha sana na viongozi wetu wema wanatuonyesha viungo vyote ; hatimaye, wanatualika dukani kama ilivyo ada.

Tunaendelea mpaka Chake-Chake kufanya ziara ya kiwanda cha kuchuja mafuta muhimu.
Mtu mwenye maringo anatuelezea matengenezo ya mafuta.
Hapa, mimea iliyoondolewa mafuta, inatumika kwa kuwasha moto.

Lucie aliazimia kubaki Chake-Chake kulala na kwenda Unguja kesho.
Kwenye kitabu cha umri wa mwaka mmoja tu, kumeandikiwa bei ya chumba cha hoteli ni dola kumi lakini, leo, mtu wa hoteli anaomba dola arobaini.
Lucie anapenda zaidi kurejea nasi Wete, kulala kwa dola kumi na kumpa yuro mbili ya kuondoka kesho kwa basi kwenda bandari ya Mkoani.
Usiku huu, hotelini, hatupewi samaki tena lakini chipsi na kuku ; hakuna chipsi nzuri Tanzania : ni chipsi nzito, nene na zilizogandamana.
Ninatamani mtandao utapatikana kesho.


yaliyomo