Jumatatu 22.06.09 : Dar-es-Salaam - Tanga


Leo tunaacha Dar-es-Salaam na basi kwenda Tanga.
Ni basi la anasa kwa watu thelathini ; inawezekana kula biscuti na kunywa juisi ya embe na maji.
Tunakutana na msichana mmarekani, biologist-paleontologist ; anafanya kazi kwenye mkoa wa Tanga na anatupendekeza kwenda kutembelea milima Usambara.
Labda tutakwenda pale.
Safari inadumu masaa sita kwa kilomita 350 na shillingi 12000 kwa mtu moja (yuro saba).
Tunafika Tanga ; ni mji mzee na unaopendeza.

Kutoka chumba cha hoteli, tunaona bahari.
Kesho, meli itakwenda kisiwa cha Pemba.
Hatutabaki Tanga siku mzima, tutaondoka kesho kwani tunaazimia kwenda Pemba.

Tunatembelea mjini, tunakula kidogo na tukanunua vitu.
Sokoni, ninanunua shokishoki nisizozijua ; ni matunda mawili rangi ya kijani, juu na upande wa kulia wa picha.
Yataiva kesho asubuhi.
Ninastaajabu kwa sababu ninaona machungwa na machenza rangi ya kijani ; kule Ulaya, hakuna.


yaliyomo