Ijumaa 26.06.09 : Wete


Leo, ni siku shwari zaidi.
Hapa, tupo katika ncha ya kusini na hali ya hewa ni joto sana na hatupati blanketi kwa kulala lakini ninahisi joto hasa awali wakati wa usiku.
Kuna mbu lakini tuna dawa na vyandarua kwa hiyo hakuna shida.
Asubuhi mapema sana, Lucie ameondoka kuelekea kusini mwa kisiwa.
Hatimaye mtandao unapatikana lakini, inabidi nifikishe yapata megabyte moja na saa moja haitoshi ...

Ni picha ya bibi anayetayarisha mboga kwa wanunuzi wa hoteli.
Tunazunguka kidogo mjini na tunavunja pesa ; hapa ofisi kwa kupata shilingi zinaitwa "bureau de change", kwa kifaransa.
Mvua inanyesha kidogo.

Nje ya soko hili, tunaona mahali inapowezekana kula.
Tunapewa aina ya chapatimaji na vipande vichache vya nyama na mchuzi.
Sio vibaya na jumla ya risiti ni shilingi 700 kwa mtu mmoja ; hatutasikitika.

Tunaazimia kuondoka kesho mpaka Mkoani, kusini mwa kisiwa.
Na daladala, ni muda mrefu na kama mgongo unaanza kuniuma, tunachagua kwenda na basi kwa sababu mwendo unadumu saa moja na nusu.
Usafiri unaanza saa tatu asubuhi ; sawa.
Na sasa, mtu anatueleza basi litaondoka saa kumi na moja na nusu alfajiri !
Ni mapema sana lakini tunakubali.
Tunatayarisha mizigo yetu lakini ... hakuna umeme tena !
Ninalala hadi saa nne usiku na umeme unarudi dakika chache tu na tunajaza sanduku na nuru ya kurunzi.


yaliyomo