Jumamosi 20.06.09 : dar-es-salaam


Mzigo unaopotea haufikishwi hotelini lakini mtu wa uwanja wa ndege anatuahidi kuuleta asubuhi.
Ingridy ananiandikia ujumbe wa simu kwa kunitaarifu anafika kutusabahi ; Noemie anakwenda kutembea mjini na mtu anamwibia noti chache. Muda huo, mimi ninamngoja Ingridy anayefika ; ana mimba kubwa (sikujua).
Tunakutana, tunaongea na tunastaajabu kwani mzigo unafikishwa hotelini.
Mimi na Noemie tunamshauri kuhusu safari yetu na tunaazimia kwenda kaskazini mashariki ya Tanzania.
Ingridy anapendekeza kutembea kesho Bagamoyo (kilomita sabini kaskazini ya Dar-es-Salaam).
Anaelekea kwake na atarudi usiku kwani ninawaalika hoteli ya chakula yeye na Christopher.

Baada ya kutoka kwake, tunaelekea soko kubwa la Dar-es-Salaam (Mnazi mmoja) lakini, bahati mbaya, limefungwa leo.
Tunakula kidogo na tunakwenda mpaka ofisi ya mabasi kununua tiketi za kwenda Tanga jumatatu asubuhi.

Hapa, hakuna wazungu wengi : tuliwaona wawili tu barabarani.

Ndugu wa Christopher anakuja kutuchukua na akatupeleka nyumbani kwa Christopher na Ingridy kwa sababu wanatualika kwao badala ya kwenda hotelini.

Ua wa nyumba yao ni mkubwa na kuna upande wa kwao, upande wa familia nyingine na upande wa ndugu wawili wa Christopher.
Huyo anatupikia vyakula vizuri : ndizi na kitoweo cha ng'ombe na samaki.
Kuna divai ya Afrika ya Kusini lakini mimi, tangu kuingia Tanzania, ninakunywa bia tu inayoitwa "Kilimanjaro" ; ni bia nzuri lakini ninapenda zaidi bia za Ubelgiji.

Tunaongea pamoja kwa kiswahili, kiingereza na kifaransa, na muda huo, luninga inaendelea kutangaza.
Inaonekana kama Ingridy amechoka ; hivyo, Christopher na ndugu yake wanaturudisha hotelini.

Hatukuzungumza kuhusu matembezi ya kesho lakini hakuna shida.


yaliyomo