Ijumaa 19.06.09 : Dar-es-Salaam
Kama ilivyokuwa Kigali, mwaka 2007, mwadhini anaanza kuimba saa kumi na moja alfajiri na kisha, kanisa katoliki karibu
na hoteli linapiga kengele na kisha watu wa kanisa wanaimba kwa sauti kama ndege.
Leo, tunazunguka kwa miguu katika Dar-es-Salaam yote.
Mchana, tunakwenda mpaka mwisho wa mto na tunaelekea soko la samaki.
![]() |
Inanuka sana ! |
Ninaongea na vijana wauzaji wa samaki na tunacheka sote pamoja.
Wanakubali ninawapiga picha na wananipa anwani ya kuwafikishia picha. |
![]() |
![]() |
Unaweza kuona picha ya kuwasili Kigamboni, kutoka ndani ya kivuko ; mwendo yapata dakika kumi |
Baada ya chakula cha usiku, ninangoja mzigo ambao karani wa uwanja wa ndege aliahidi kuniletea leo.
Msichana wa hoteli ananiambia kuwa ataniwekea mzigo ili niweze kulala sasa.
yaliyomo
![]() |
![]() |
![]() |