Alhamisi 18.06.09 : Ottignies-Louvain-la-Neuve - Dar-es-Salaam


Anne anaamka mapema kutupeleka katika uwanja wa ndege.
Maneno ya kwanza ya karani wa kaunta ya mizigo ni : "ninakukumbuka, wewe, ni mwanamuziki !"
Lakini haniombi sahihi yangu.
Sisadiki kwamba nitakaribishwa hivyo Dar-es-Salaam.
Mruko wa KLM una vituo vitatu : Brussels - Amsterdam kwenye Fokker 70 kisha Amsterdam - Kilimanjaro na mwishowe Kilimajaro - Dar-es-Salaam ndani ya Boeing 777-200ER.
Mimi na Noemie tunapewa viti mbalimbali lakini kwa kuwa ndege haikujaa, tunaweza kubadili nafasi : yeye anakaa peke yake kwenye msafa wa viti viwili karibu na dirisha na mimi anakaa peke yangu kwenye msafa wa viti vitatu karibu na dirisha.

Mruko juu ya Libya unanikera kwani ni jangwa daima. Niliposafiri juu wa Uholanzi niliona nyumba nyingi, mimea na maji.
Lakini kati ya jangwa, tunaona sanamu za kiajabu katika mchanga.
Baada ya kurudi nyumbani, nikagundua huwa : ni mashamba karibu na mji wa Koufra (24°05'N 23°15'E).

Mimi na Anne tulikutana na msichana mtanzania hapa Ubelgiji anaitwa Ingridy ; nilimweleza kuhusu kuwasili kwetu na alisema mume wake (Christopher) atatupokea uwanja wa ndege Dar-es-Salaam.
Mzigo mmoja haukuwasili na karani anatueleza mzigo umebaki Amsterdam.
Ninatembea mpaka mlango wa kutoka na ninakutana na Christopher akiwa na karatasi limeandikwa "Bubu" (ni jina langu la kupanga).
Alikuja pale na rafiki yake na wanatuendesha mpaka hoteli ya YMCA.
Tulikuwa na mizigo mitatu : mzigo wangu, mzigo wa Noemie na mzigo wa zawadi kwa Ingridy.
Mzigo wa tatu atatuletea kesho katika hoteli na hivyo, nitaweza kumpa Ingridy mwenyewe. Ingridy hakuja uwanja wa ndege kwa sababu sasa anafanya kazi Morogoro na atarudi jumamosi.
Inabidi tujaze fomu kuhusu upotevu wa mzigo na kazi hii inadumu saa moja.
Kwa hiyo, tunafika hotelini baada ya kufunga, lakini tunafanikiwa kukutana na mtu anatusaidia kumtafuta msichana wa hoteli anayekubali kutupokea.
Chumba safi na hakina anasa


yaliyomo